HIJAMA (CUPPING THERAPY)
KSh 3,900.00
♥️-HIJAMA (KUUMIKA) [cupping therapy]
🟢-hii ni tiba ambayo imekuwa ikitumiwa tangu jadi kwa lengo la kutibu maradhi mbali mbali kwa njia ya kutoa damu chafu mwilini
🔺-MAANA YA HIJAMA
Neno Hijama linamaanisha ‘kutoa’ kwa Kiarabu. Kwa sasa inatambulika kama njia mbadala ya tiba ya kutibu maradhi mbali mbali na magonjwa mengine katika mwili.
💢-Hijama au kuumika ni salama, isiyokuwa na madhara na njia isiyogharimu katika kutibu na kuzuia maradhi.
⚫-FAIDA YA HIJAMA
Faida ya kwanza kabisa na inayoongoza ya kuumika au hijama kwa muumin ni faida atakayoipata hapa duniani na kesho akhera, baada ya kufuata sunna iliyokokotezwa ya Mtume Muhammad
🟥-FAIDA ZAIDI
Inafahamika kwamba kuumika au hijama inasaidia kuongeza nguvu katika damu.
1️⃣- Inaondoa sumu na uchafu katika damu.
2️⃣-Inaharakisha uponyaji wa haraka na watu hupona maradhi haraka baada ya kuumika au hijama.
3️⃣- Kuumika au Hijama inafahamika kwa kuzuia maradhi na kwa hiyo inaweza kusadikika kama inaongoza katika ukingaji wa maradhi mengi.
4️⃣-Zaidi ya hayo, pia ianfahamika kwamba kuumika au hijama inaweza kuwasaidia wale watu ambao wamekumbwa na uchawi au wamepatwa na Jini.
NB
✅-“Dawa iliyobora ambayo unaweza kujitibia ni kuumika, au ni miongoni mwa dawa bora kabisa au Dawa unaweza kuitumia ni kuumika.”(Sahihi Bukhari:5371)
Njoo upate huduma hii kwa wanaume na wanawake






